KIVULI CHA ALLAH(S.W) SIKU YAKIAMA
"Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kuna watu saba (7) ambao Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) atawafunika katika kivuli chake katika siku ambayo kutakuwa hakuna kivuli isipokuwa kivuli chake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)”:
1. Kiongozi Muadilifu
2. Kijana aliyekulia katika kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)
3. Muislamu ambaye moyo wake umesehelea katika msikiti
4. Watu wawili wapendanao kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), Kukutana kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na kuachana kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)
5. Mwanaume aliyeitwa na mwanamke mrembo kwa kutaka kufanya matendo ya haramu na akasema, “La hakika mimi namuogopa Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)”
6. Mtu anayetoa sadaka kwa mkono wa kulia na wa kushoto usijue kitu kilichotendeka (atoae sadaka kwa siri bila ya wengine kujua kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)
7. Mtu anayemkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa faragha na huku macho yake yakatokwa na machozi.”
(Al-Bukhaariy na Muslim) Katika Hadiyth hii nzuri Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kazungumzia kuhusu vitu vidogo vya ‘Ibaadah ambavyo ujira wake ni mkubwa mno: kivuli katika siku ambayo kutakuwa hakuna kivuli isipokuwa cha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Hii inaweza kuonekana kuwa si jambo kubwa katika mara ya kwanza utakaposoma, lakini ukidhamiria katika Hadiyth ifuatayo; “Katika siku ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) atawafufua viumbe vyake vyote, jua litashushwa karibu sana na watu ambapo kutaachwa tofauti ya maili moja baina ya jua na watu ardhini. Watu watatopea katika jasho kulingana na amali zao, wengine mpaka kwenye vifundo vya vya miguu, wengine mpaka kwenye magoti yao, wengine mpaka kwenye viuno vyao na wengine watakuwa na hatamu ya jasho na, wakati yalivokuwa yanasemwa haya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliweka mkono mbele ya mdomo wake.” Imesimuliwa na Al-Miqdaad bin Aswad na imekusanywa katika Swahiyh Muslim - Juzuu ya nne (4), ukurasa wa 1487-8, nambari 6852.
TUOMBEE ZAIDI TUWE NA TABIA HIZI.
TUWEKE MAZINGATIO
13 years ago