BISMILLAHI RAHMANIR RAHIIM
MADA: MAENDELEO DUNI YA KIELIMU KWA WAISLAMU WA TANZANIA NI YA KIHISTORIA
Ndugu zangu katika imani, tathimini ya elimu katika nchi yetu katika cha hivi karibuni inaonyesha kushuka. Kwa mfano mwaka 2011 katika matokeo ya kidato cha nne inasemekana karibu 50% ya wanafunzi wamefeli mtihani. Lakini cha kusikitisha zaidi waathirika wakubwa wa matokeo hayo ni wanafunzi wa serikali za kata.
Hali hii inatugusa sana sisi waislamu kwani kwenye sekondari hizo za kata ndiko wanakopatikana wanafunzi wa kiislamu wengi. Utafiti unaonyesha kuwa katika sekondari nyingi maalum zenye hadhi ya kiwilaya na kitaifa idadi ya waislamu ni kama 10% tu. Sisi wasomi wa ngazi zote kuanzia sekondari, vyuo mbalimbali na vyuo vikuu tunatakiwa kulitathimini hili kwa kina, kwani Allah (S.W) anatueleza kuwa:
“Wala haiwapasi waislamu kutoka wote (katika miji yao) lakini kwanini halitoki kundi (tu) katika kila taifa miongoni mwao (liende) kujielimisha vyema dini na (kisha) wakaja kuwaonya wenzi wao (waliosalia makwao) watakaporudi, ili wapate kujihadharisha (na wabaya wao)”
Qur’an 09:122
UFAFANUZI
Kujielimisha dini- Ina maana ni elimu yoyote ile ya mazingira na ya kiroho, zikiwemo hizi za kimazingira tunazozisoma (sharti tusipotoshe ukweli). Kwa maana hiyo tuna wajibu wa kuinusuru jamii kutokana na elimu tunayoipata, ikieleweka wazi kuwa sisi (wasomi wa kiislamu) tunauelewa mkubwa kuliko ndugu zetu katika imani tuliyowaacha katika maeneo mbalimbali ambao hawajabahatika kupata neema hii ya elimu kama sisi.
Swali la kujiuliza ni, kwa nini asilimia ya waislamu ni ndogo sana kuanzia sekondari, vyuo mbalimbali mpaka vyuo vikuu ukilinganisha na wakristo?
Jibu la swali hili linapatikana kwa kuangalia historia sahihi ya nchi yetu kuanzia wakati wa ukoloni mapak baada ya uhuru.
Tunaanza kurejea historia hii kwa kumtumia msomi wa kiislamu Sheikh K.S Kiangi Msuya, ambae alielezea juu ya udhalili wa elimu kwa waislamu wa Tanganyika. Maneno yake yalichapishwa katika gazeti la KIONGOZI la tarehe 26-Oct-1956 chini ya kichwa cha habari “udhalili wa elimu kwa waislamu Tanganyika”. Inasemekana kuwa hesabu ya watu wa Tanganyika ni zaidi ya 8,102,000 na katika hesabu hii waislamu ni zaidi ya 4,500,000. Sasa nataja shule zote uonekane udhalili ulioko juu ya waislamu:
HESABU YA SHULE ZOTE TANGANYIKA 1955.
1.(a) Shule za Msingi za Utawala (Government Primary School) ni 656
(b) Shule za Msingi za Wakristo ni 1692
(c) Shule za Msingi za Kiislamu ni 28
2.(a) Shule za Utawala (Government Rural Middle) ni 104
(b) Shule za Wakristo Rural Middle ni 223
(c) Shule za Waislamu Rural Middle ni HAMNA
3.(a) Shule za Sekondari za Utawala (Government Secondary School) ni 10
(b) Shule za Sekondari za Wakristo ni 16
(c) Shule za Sekondari za Waislamu ni HAMNA
4.(a) Shule za Ualimu za Utawala (Government T.T.C) ni 7
(b) Shule za Ualimu za Wakristo ni 23
(c) Shule za Ualimu za Waislamu ni HAMN A
5.(a) Shule za Ufundi, Utibabu n.k za Utawala ni 7
(b) Shule za Ufundi na Utibabu za Wakristo ni 5
(c) Shule za Ufundi na Utibabu za Waislamu ni HAMNA
Shule hizi hapo juu huendeshwa na kwa fedha tulipayo kwa kodi na ushuru wa watu wote wa Tanganyika na muislamu akihitaji kuingia katika shule za sekondari ama za ufundi za wakristo huambiwa abatizwe awe mkristo ndipo atakubaliwa kusoma hapo. Pia shule za Kati (Middle School) 104 za Serikali ambazo serikali inasema inapokea watu wote, sivyo kabisa kwani ataingiaje Shule ya Kati wakati hajapita katika Shule ya Msingi?
Kwa mfano Kibohehe, Machame wilaya ya Moshi ina wanafunzi 140, kati yao waislamu ni 12 tu na wakristo ni 128, kuingia Shule za Sekondari na za Ualimu itakuwaje? Wanafunzi wa Tanganyika waliongia chuo cha Makerere 1950-1955 ni 500, ila waislamu katika watu mia ni watano tu na 95 ni wakristo, hivyo waislamu watapataje maendeleo?.
(Seikh K.S Kiangi Msuya)
Yaani wakristo walikuwa wana neemeka huku waislamu wakinyonywa, kupuuzwa na kudhalilishwa. Kwa kugundua hilo ndio maaana waislamu walianzishwa harakati za kupambana na wakoloni, rejea upinzani (resistance) karibu zote, mfano:-
•Vita vya majimaji
•Vita vya Mkwawa dhidi ya Wajerumani
•Mtemi Mirambo wa Tabora
•Abushiri bin Salum na wengineo wengi
Pia walianzisha TAA 1929 na baadae wakaanzisha Al-Jamiaul Islamiyya 1940 na hatimaye TANU 1954 (hawa wote walikuwa ni waislamu). Waliamu kumkaribisha wakristo akiwemo J. K Nyerere, ni hapo ndipo walipofanya kosa kwani waliisahau aya ya Allah (S.W) inayosema:
“Hawatakuwa radhi juu yenu, mayahudi na manaswara mpaka mfuate mila zao” (QUR’AN 2:120)
Wakristo hawa waliitumia nafasi ile kujiimarisha na kuanza kujipanga kimaslahi yao zaidi. Kwa pamoja wakoloni na wakriso wa Tanganyika wakatumia nafasi hiyo kumuandaa ili aje kuwa kiongozi wa nchi na pia kuwaandaa wakristo wengine ili waje kuwa viongozi wa baadae.
Padri Paul Crane alidhihirisha siri hii alipotembelea Tanganyika aliposema “Lazima tujitahidi kadri ya uwezo wetu kupata wasomi wakatoliki ambao watashika nafasi muhimu zote za kijamii” haya yanapatikana katika kitabu Paul Crane “Problems of the movement of the young away from the Churc” Kimechapishwa ROME, CIPA 1960.
Kwa hiyo baada ya uhuru alichokifanya Nyerere ni kutekeleza maazimio waliyoyaweka ndio maana yeye mwenyewe amenukuliwa katika kikao cha siri kati yake na viongozi wake wa dini, katika kitabu cha “Development and Religion in Tanzania” Ukurasa 333, 335 akisema:
“Tanzania sio nchi ya kikatoliki lakini ukatoliki una nguvu. Kawaambieni maaskofu, nimeunda idara ya elimu ya siasa katika TANU nimemuweka mchungaji wa Kilutheri aiongoze, yeye sio mahiri katika siasa lakini nimemuweka kwa sababu ya imani yake madhubuti na katika kamati kuu nimeweka wachungaji wawili. Naamini hii ndiyo njia nzuri ya kupata watu katika chama”
Kwa hiyo baada ya uhuru waliouhangaikia, waislamu walianza kubaguliwa na kunyimwa haki zao. Ndipo waislamu walipoamua kujiunga na waislamu wenzao wa Afrika Mashariki na kuunda EAST AFRICA MUSLIM WELFARE SOCIETY (E.A.M.W.S). Mwaka 1964 waislamu kupitia E.A.M.W.S wakiongozwa na waziri wa Nyerere (aliyekuwa Mwenyekiti wa A.E.M.W.S-Tanganyika) walienda Misri na nchi nyingine za kiislamu kutafuta msaada wa kujenga chuo kikuu cha kiislamu. Serikali ya Misri iliahidi kujenga chuo hicho kikuu na kwamba kingesimamiwa na E.A.M.W.S. Waliporudi waliitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kwa kirefu mafanikio waliyoyapata.
Kanisa halikufurahishwa na hali hii lilimtumia J. K Nyerere kufanya yafuatayo:
1)-Nyerere alifanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na kumpeleka Tewa Said Tewa kuwa Balozi wa China (ili kuvunja harakati).
2)-Alipandikiza migogoro E.A.M.W.S na hatimaye ikavunjika
3)-Akaanzisha BAKWATA mwaka 1968
Kwa hiyo matatizo yote ya kiuchumi na kijamii tuliyonayo waislamu chanzo ni kanisa, hasa katoliki likishirikiana na viongozi wao wa serikali. Hali ilivyo hivi sasa baada ya miaka 50 ya uhuru kwetu waislamu inatisha zaidi. Katika sekondari zote zenye sifa, vyuo mbalimbali pamoja na vyuo vikuu uwiano ni wakristo 90% na waislamu ni 10%. (Huu ni uwiano kwa shule na vyuo vya serikali) lakini wao wana shule nyingi na vyuo vingi. Mfano, wakati serikali inavyuo vikuu visivyozidi 10, waislamu bara wana chuo kimoja, wakristo wana vyuo zaidi ya 30 ukujumlisha na matawi yao. Je hali itakuwaje masiku yajayo???
Kinachotushtua zaidi ni manma hilo kanisa linavyolalamika kila kukicha kuwa serikali inawependelea waislamu na hawakuishia hapo tu bali walitoa na nyaraka mbalimbali za kukiunga mkono chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA. Si kwamba ninalengo la kuipinga CHADEMA bali nataka tuwe makini kwa kujiuliza hivi, ikiwa chama cha TANU kilichoasisiwa na waislamu toka TAA walikaribishwa na wakakichakachua na mpaka sasa ni CCM ambacho wanatudhulumu hadi hivi sasa, Je kwa chama hichi wanachokiasisi chenyewe (wanachokianzisha Wakatoliki)?
Ushahidi mmoja namna wakristo wanavyohusika na CHADEMA ni wa gaeti la MTANZANIA namba 5180 la Julai 21, mwaka 2010, kichwa cha habari ni “Dr. SLAA KUGOMBEA URAISI” (maandishi madogo) “anategemea udini wa wakristo kushinda” Mwandishi ni (Mageresi Paul)
Cha kusikitisha zaidi wanatumia elimu waliyoipata kuwarubuni waislamu wengi wawape nguvu na ndio hii inayoitwa NGUVU YA UMMA.
Mifano:
1)-Kati ya wafuasi wawili wa CHADEMA waliokufa katika vurugu za Arusha mmoja ni muislamu Bw. Ismail Omari (Miaka 25).
2)-Mfanyabiashara muislamu Mustafa Sobodo alitoa Milioni mia moja (Tsh. 100,000,000/=) mara mbili tofauti kwa CHADEMA na kufanya jumla ya Tsh. Milioni mia mbili (Tsh. 200,000,000/=).
Ieleweke hatuna nia ya kumchagulia mtu chama cha siasa cha kukifuata, bali tunataka waislamu wachukue tahadhari popote watakapokuwepo, kwani historia inaonyesha kuwa wasio waislamu wanataka vyote bila ya kuwafikiria/kutufikiria sisi waislamu. Ni wajibu wetu kuitumia elimu tuipatayo ipasavyo ili iweze kutukomboa na pia kuwakomboa wengine. Allah amesema katika Qur’an 09:122
“Wala haiwapasi waislamu kutoka wote (katika miji yao) lakini kwanini halitoki kundi (tu) katika kila taifa miongoni mwao (liende) kujielimisha vyema dini na (kisha) wakaja kuwaonya wenzi wao (waliosalia makwao) watakaporudi, ili wapate kujihadharisha (na wabaya wao)”
WABILLAH TAWFIIQ
By K/Habari
BILAL KHALID
TUWEKE MAZINGATIO
13 years ago