بسم الله الرحمن الرحيم

kutafuta elimu ni faradhi kwa kila muislamu
الحمد لله الذي نستعينه ونستغفره ونعوذ بالله من شرور أنفسنا ومن سيئات أعمالنا من يهد الله فلا مضل له ومن يضلل فلا هادي له .



ونشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له ونشهد أن محمدا عبده ورسوله أرسله بالهدى ودين الحق ليظهره على الدين كله وكفى بالله شهيدا




Wednesday, April 13, 2011

KWANINI UISLAMU UMERUHUSU KUOA MKE ZAIDI YA MMOJA?.

Swali hili twaweza liuliza hivi: Kwanini wanawake hawafai kuolewa na mume zaidi ya mmoja,ila wanaume wamepewa ruksa ya wake wanne?
Hili linabainishwa kwa aya ya mwenyezimung ifuatayo:

[Anisaa:3]
“Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana”.
ALLAH ameruhusu mwanaume kuoa mke zaidi ya Mmoja na si mwanamke kuolewa na mwanamme zaidi ya mmoja kwani yeye(mwanamke )anahifadhi bacteria na virusi vinavyojengeka na mwili wa mwanadamu wapatikanao katika manii ya mwanaume na hivyo kimaumbile akihifadhi bacteria na virusi vya zaidi ya mwanamme mmoja ataleta madahara yafuatayo:
1. Ataleta mapiganao aya viumbe bacteria katika mfumo wake wa uzazi ulio na tabia ya kimaumbile kuyapokea na kuayahifadhi kupitia mfumo wake wa uzazi bacteria hawa ni pamoja na mjengo acidi uoneshao asili ya mwanadamu na kitambulisho cha mtu uitwao DNA(Deoxyribonucleic Acid) utaokanao na kujengwa na damu,mate na mbegu za kiume za mwanadamu. Bacteria hawa wakipigana hufa miongoni mwao kuleta uozo ujengao Neisseria gonorrhoeae na wengine hujengwa waitwao Chlamydia trachomatis, Treponema pallidum ,hukimbilia katika sehemu ya ndani ya mfumo wa uzazi kupitia nyama laini inayoujenga mfumo huo hivyo kuleta MAGONJWA kama klamadia,kaswende,kisonono na maumivu, hali hii na athari zake hujijenga na kuwa mabaya zaidi endapo itakuwa mapigano ya bacteria wa namna tofautitofauti kutokana na mwanamke kushiriki jimai na wanaume wengi.

2. Pia kutapatika muingiliano baina ya virusi mwili na kuzaliwa/ kujengwa virusi wapya wenye madhara waitwao kitaalamu herpes simplex virus(HSV) wasababishao ugonjwa wa malengelenge na hatari zaidi ni kupatiakana kwa Human immunodeficiency virus (HIV) washambuliao kingamwili.

Kulazimika kwa ndoa katika uislamu kuna hekma kubwa ambayo huyaepusha haya na pia kuyaepusha haya Allah (sw) amewalazimisha wanawake na wanaume kudumu katika jimai ya ndani ya ndoa. Mwanamke anapokea viambato vya mwanaume mmoja tu kwa namna ya maumbile aliyowaumbia Allah (sw) na sikinyume na hapo, kuyaasi haya ndipo zinakuja adhabu za mungu zinazotibika na zisizo na tiba kama UKIMWI.
Wataalamu wanasemaje katika uwezo wa uzalishaji na haja ya jimai:
Mwanaume wakawaida mwenye nguvu, mzima wa mfumo wa uzazi ana uwezo wa kuwahudumia wanawake watatu hadi wane kwa haja zote mbili za kuwatosheleza kwa mahitajio na akshi za kimwili pia kwa majenzi ya uzazi na kuzaliana, kwani wanaume wameumbiwa uwezo wa kutengeneza mbegu na mshindo wa jimai zaidi kuliko wanawake.
ALLAH AALAM.
YAMEKUSANYWA NA SULEIMAN ABDALLAH.

KWANINI MANII SIO NAJISI LAKINI MKOJO NI NAJISI?

MAKALA HAYA YANAENDELEA KUTOKA MAKALA YA KWANINI TUNAOGA JANABA
Manii si uchafu wa najisi kwa mjengo wake aliotuumbia Allah bali uchafu wa hali na kinai kwa ilipodondokea na hii ni kwa matashi ya binaadamu.
Turudi kutazama manii ni nini?
Manii ni kimiminika kijulikanacho na kubeba tafsiri ya lugha ya kitaalamu kama “SEMEN” kitolewacho (ifahamike manii hutolewa hayatoki yenyewe kama madii) na sehemu ya uume kwa mwanaume kama matokeo ya mshindo, mshushio, na upeo war aha na nakshi ya jimai ifahamikayo kitaalamu kama “Orgasm” na huwa na viambato na tabia zifuatazo:

A. Manii ndani yake kuna mbegu (sperms):
i. Mbegu hizi ndio asili ya uzazi na mjengo wa mwanaadamu zinatengenezwa katika makende (nje ya joto la ndani ya mwili). Mbegu hizi hujengwa na vitu viwili Chromosomes na gamates or male germ cells zenye Cytoplasm, vitu hivi viwili ni viambato vinavyopatikana katika vipimo vya DNA. (kuna X-chromosomes na Y-chromosemes)
ii. Katika mbegu hamna asili yeyote ya uchafu wala najisi bali katika vitu viwili tulivyovitaja hapo juu kuna vaiambato kama Vitamin (C&B12), Madini (Calcium, Magnesium, Pottasium, Phosphorus na Zinc) na Sukari(Fructose na Sorbito).
iii. Mbegu zenye manii ndizo zitolewazo, hazitoki zenyewe katika mwili wa mwanaume, sababu na kazi ya mbegu katika manii ni kupevusha mbegu za kike (Ova) katika jimai mgegu katika manii ni 10% tu.
iv. Mbegu (sperms) ifahamike kuwa ndani ya makende/korodani huhifadhiwa katika kiungo mfano wa koili kwa siku mwanaume mwenye afya hutengenza kati ya mbegu 70-150 milioni na huchukua wiki 10 mbegu 1 kupevuka na mbegu zilizopevuka katika koili hiyo hukaa takribani masiku 40 kabla ya kutolewa au kuvunjwavunjwa na kufyonzwa na mwili. Hapa tunajifunza na kugundua hamna haja ya kuzitoa mbegu kwa nji mbadala kama wanaotetea na kutoa elimu ya Punyeto, kwani Mola katuumba vema hamna haja ya kuvuka mipaka.Manii haijengwi na mbegu pekee bali pia kuna viambato kama ifuatavyo;

B. Manii pia ndani yake kuna kiambato krozomu kiitwacho “Seminal Plasma” kiambato hiki hutokana na maji yajijengayo na kutokana na damu ni kiambato kikubwa na muhimu katika manii huchukua zaidi ya 60% , kiambato hiki kipo katika hali ya kimiminika na hutolewa na tezi za mwanaume ziitwazo “Prostate Gland” zenye muundo wa “O” zizungukazo katika tundu mkabala na la mkojo. Kiamabato hiki hulinda mbegu na kuilisha kipindi cha safari yake ndefu mpaka katika mbegu za kike
NB: Eneo la mfumo wa uzazi wa mwanamke lina tindikali (acids) mno kwa kiwango ambacho seli za mbegu za kiume kuhimili maisha/kukaa na hivyo ndani ya “seminal Plazma” kuna viamabato vingi vya Alkalini vinavyoshindana na Acid ila ni kwa uchache mafanikio huwa na kwa namna hiyo mbegu chache hufika katika kupevusha yai la mwanamke, mara nyingi moja na kwa uchache mbili,tatu au nne kwa mapenzi ya Allah(sw).
Alkali iliyopo hapa hulinda gamets za kiume.
C. Manii pia ndani yake kuna tezi viambato ziitwazo “Seminal Vesicle” ambazo huyapa manii nguvu ya msukumo huyabeba seminal plasma tezi hizi hukaa pamoja na golegole /utelezi au kamasi/ute/utando utokanao na maji ya damu ambayo huizunguka mbegu ute huu ndio wenye protini kama chakula cha mbegu katika safari yake hadi katika ukuta wa uzazi.
Katika manii kuna viamabato kama “CITRIC ACID, “Kwa yakini mchanganuo wa kikemia wa kimiminika hiki manii, umedhihirisha kwamba pamoja na vitu vingine unahodhi kiwango kikubwa cha “phosphoric acid” na “calcic acid”. Na zote mbili hizi ni maada kima zenye taathira adhimu katika ujenzi wetu wa kimwili (kama wanadamu). Sodium na Zinc” pia kuna “Enzymes” hufanya sehemu ya asilimia zilizobaki, viamabato hivi utokaji wake hupita katika mishipa ya mwili na kuipasha ua kuichoma kwani vina moto na tindikali.

Nukta hii hutuleta Katika pointi ya msingi ya kujibu swali letu la msingi

Kwanini tunaoga Janaba?
“Kwanini tunaoga kwa kutokwa na manii ambayo si najisi”

Katika VIAMBATO hivi vya mwisho vya manii ndivyo hekma ya kitaalamu ya kupatikanika kuoga, kwani kwa athari ya mishipa ya mwili kuchomwa na maji ndicho kiungo pekee kinacho kuwa na uwezo wa kuipooza na kuipa nguvu yake ya asili, ifahamike kuwa :-
Kitaalamu maji ni muunganiko wa hewa mbili yaani “Hydrogen mbili (H2) na Oxygen moja (O) = H2O. Hivyo kwa zoezi la kushusha manii hufanya nguvu kutumika na husimamisha vinyweleo baada ya kumalizika zoezi lile katika kipindi hicho vinyweleo huwa wazi, hivyo unapooga maji hewa ile ya Oxygen na Hydrogen husafiri kwa kupitia vinyweleo kwenda kuiipooza mishipa na athari ya Acid na viambato vya mpito wa enzymes. Hivyo Allah akatutaka kuoga sio kuwa antuonea bali kwa kuwa ndiye aliye tuumba antufahamu na hatuna budi kuifuata amri yake hii ya sura ya 5 (Almaidah):6.
Acid hii ipatikanayo katika manii ni aina ya Citric yenye sifa za kelegeza baada ya kuchoma tokea yanapojikusanya hadi kutoka kwa aitoaye na inayemwingia pia hivyo hekma ya maji pia ni katika kurudisha nguvu ya mwili yaigusapo ngozi, Wataalamu wanatushauri kwa janaba tuoge maji ya kati yasiyo baridi sana kuliko ya moto kwalengo la kuirudisha hali ya mwili vema.

Hekma ya kutowaingilia wanawake nyuma na athari kwa Mashoga.
Wanaume wanaoingiliwa (mashoga) huathiriwa na kulegezwa na acid hii na pia kwa kupatikana virus wanaokosa mahali pakwenda kukaa hivyo hukosa haiba ya ukakamavu wa kiume na kuwa na haiba na mihemuko ya kike haya huwa matokeo ya athari za viambato alivyoumba mungu kwenda kukaa mahali Fulani kwenda kuwekwa kwengineko vivyo hivyo kwa wanawake waingiliwao nyuma Allah amekataza, kwa kufanya hivyo kitaalam kuna athari kubwa kwani hmna makazi sahihi ya viumbe/viambato alivyowaumba katika manii.

Kwanini manii si najisi?
Pia turejee swali letu linguine la msingi juu ya Utambuzi wa kunajisika manii:
“Je manii kwanini si najisi?”
Katika muda wa kipindi cha msisimko na hisia za kijinsia(mapenzi) na mahitajio pia wakati wa kufika kileleni manii husafirishwa na nguvu ya seminal vesicle tulizozizungumzia juu kama tezi viambato husafirishwa kwa njia ya mirija iitwayo “Vas Deferens” hivyo hayanajisiki kwa namna yeyote japo huonekana kutoka katika njia moja na mkojo, kinachofanyika kwa yale maji yanayotoka kabla ya manii yenyewe huwa najisi nay ale maji yanayotoka pekee bila manii huwa najisi vilevile(hapa ni katika pointi ya madhii na madii) kwa kupita njia isiyo mrija wa Vas Deferens. Katika njia ya Vas Deferens manii hupata kimiminika chenye kuwa na Sukari ya Fructose inayoongeza nguvu ya msukumo kama mafuta ya roketi (Bit like Roket fuel) na pia kuingiwa na tezi kama Prostate gland, Cowper gland pamoja na hiyo Seminal vesicle gland, tezi hizi hupunguza nguvu ya tindikali itokayo katika njia ya uchafu na nguvu ya mwili na pia mkojo hivyo kuifanya manii kuwa safi na salama itokapo, haiwezi kuwa najisi huu ndo ukweli juu ya manii kwa mujibu wa wataalamu pitia kitabu cha “Science; Spermatogenesis in Man, An Estimate of Its Duration” By Dr. C.G. Heller 1963 (Armenia medical Network) ..

ALLAH AALAM.
YAMEKUSANYWA NA SULEIMAN ABDALLAH.

KWANINI TUNAOGA JANABA?

Kwanza kabla sijafafanua tujue kabisa kuoga Janaba ni amri ya Allah ipatikanayo katika kitabu chake kitukufu isemayo:
....وَإِنْ كُنْتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُو......(5:6)
((Na mkiwa na janaba basi ogeni)) [Al-Maidah :6]
Sasa tutazame kwa nukuu na swali lifuatalo kisha tutaeleza kitaalamu hekima ya mafunzo na shuruti hii ya kuoga janaba.

Kuna swali liliulizwa katika tovuti ya www.alhidaaya.com kuhusu janaba na kuoga kwake nalinukuu kama lilivyo tuweze kupata faida zaidi:
SWALI:
Naomba inshaallah unieleze kidogo namna ya wanawake wanavyotakiwa kuoga janaba baada ya maangiliano na mumewe. Kwa sababu jambo la kuingiliana baina ya mume na mke linafanyika kila bada siku chache tu, sasa kwa vile wanawake wanajisikia uzito kuosha nywele kila siku kichwa kizima, kwa sababu ni jambo la mara kwa mara bila shaka kuna tofauti na kuoga baada ya wanawake kupata period au baada kujifunguwa.
Tulikuwa na shekh mmoja na kwake tulisoma hii habari namna ya kuoga wake zetu baada ya maangiliano,lakini sikumpata sawa sawa, kwa kumbu kumbu zangu alitusomesha kwamba just wanaweza kupaka kwenye kichwa, kwa kutia maji kwenye mikono halafu wakatiya vidole chini ya mizizi ya nywele, (hii ni baada ya maangiliano sio muogo wa baada ya period au kuzaa) na akanukuu kwa kuitaja ile aya inayosema, kwani dini hii ya Kislamu ni rahisi .
________________________________________
MAJIBU:
Kuna Mas-ala mawili hapa katika Swali hili nayo ni:
1) Ghuslu ya Janaba ni sawa na ya Haydh na Nifaas?
2) Vipi mwanamke afanye Ghuslu ya Janabah?
Mas-ala ya kwanza:
Ghuslu ya Janaba, ya Haydh na Nifaas yote ni moja tu nayo ni kuosha viungo vyote vya mwili kutokana na kauli ya Allaah سبحانه وتعالى :
وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُواْ
((Na mkiwa na janaba basi ogeni)) [Al-Maidah :6]
Vile vile:
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُواْ النِّسَاء فِي الْمَحِيضِ وَلاَ تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىَ يَطْهُرْنَ
((Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka watwahirike))[Al-Baqarah: 222]
Kutoharia ni maana pia kukoga
Na dalili kwamba kujitia tohara ni kukoga imo katika aya hii:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَقْرَبُواْ الصَّلاَةَ وَأَنتُمْ سُكَارَى حَتَّىَ تَعْلَمُواْ مَا تَقُولُونَ وَلاَ جُنُبًا إِلاَّ عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىَ تَغْتَسِلُواْ
((Enyi mlio amini! Msikaribie Sala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema, wala hali mna janaba – isipo kuwa mmo safarini – mpaka mkoge)) [An-Nisaa: 43]
Kwa hiyo ni wazi kwamba kukoga (ghuslu) ni kuosha viungo vyote vya mwili.
Taratibu ya Ghuslu:
Kwanza kabisa ni kutia 'Nia' ambayo inawekwa moyoni wala haitajwi kwa kusema au sivyo itakuwa ni kitendo cha Bid'ah.
Kisha ni kujisafisha vizuri na katika Haydh na Nifaas mwanamke ajisafishe na 'Misk' mwishowe baada ya kujimwagia maji ili atoe athari ya harufu ya damu chafu katika sehemu zake.
Ghuslu ya Janaba kama alivyokuwa akifanya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
1. Kuosha mikono mara tatu.
2. Kuosha sehemu za siri
3. Kufanya wudhuu kama wudhuu wa Swalah.
Wakati mwingine Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akichelewesha kuosha miguu mpaka mwisho kama ilivyokuja katika hadiyth nyingine.
4. Hakikisha maji yanaingia katika nywele kwa kugusisha utosi mara tatu.
5. Jimwagie maji mwili mzima kwa kuanzia upande wa kulia, kisha wa kushoto, na kuosha chini ya kwapa, masikioni, pembeni mwa sehemu za siri, katika vidole vya mguu na sehemu zozote nyingine za mwili zilizokuwa wepesi kusugua. Hii kutokana na hadiyth kutoka kwa bibi 'Aishah رضي الله عنها
عن عائشة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم كان إذا اغتسل من الجنابة يبدأ فيغسل يديه،
ثم يفرغ بيمينه على شماله فيغسل فرجه ثم يتوضأ وضوءه للصلاة ، ثم يأخذ الماء ويدخل أصابعه في
أصول الشعر حتى إذا رأى أنه قد استبرأ حفن على رأسه ثلاث حثيات ، ثم أفاض على سائر جسده
، رواه البخاري ومسلم
Kutoka kwa bibi 'Aishah رضي الله عنها kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipokuwa akioga Ghuslu ya Janabah alianza kwa kuosha mikono, kisha akijimwagia maji kuanzia mkono wa kulia na kwenda mkono wa kushoto, na akiosha sehemu zake za siri, akifanya wudhuu wa Swalah, akijitia maji kichwani na kufikisha kwa vidole vyake katika mizizi ya nywele mpaka aone kuwa ngozi imeshika maji, kisha akijimwagia maji kichwani mara tatu na kisha mwili mzima. Al-Bukhari na Muslim
وفي رواية لهما : ثم يخلل بيديه شعره ، حتى إذا ظن أنه قد أروى بشرته أفاض عليه الماء ثلاث مرات
Na katika riwaya imesimuliwa: 'alikuwa akipitisha vidole vyake kwenye nywele zake mpaka anahakikisha kuwa maji yamegusa ngozi kisha akijimwagia maji mwili mzima mara tatu
Ghuslu ya mwanamke pia huwa ni sawa na ya mwanamume isipokuwa kama mwanamke ana nywele zilizosukwa hana haja ya kuzifungua bali ni kujimwagia maji na kuhakikisha maji yanagusa ngozi. Lakini kama ana nywele nyingi sana na zimesukwa kwa kukazwa sana basi ni bora afungue ili kuondoa khofu ya kutokufika maji katika nywele zote na ngozi.
أم سلمة رضي الله عنها ، أن امرأة قالت يا رسول الله ، إني امرأة أشد ضفر رأسي ، أفأنقضه للجنابة ؟ قال :( إنما يكفيك أن تحثي عليه ثلاث حثيات من ماء ثم تفضي على سائر جسدك ، فإذا أنت قد طهرت ))) رواه أحمد ومسلم والترمذي وقال : حسن صحيح
Ummu Salamah amesema kwamba mwanamke alimwambia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم "Ewe Mtume صلى الله عليه وآله وسلم mimi ni mwanamke mwenye nywele nyingi nzito zilizosukwa, je, inanipasa nizifungue ili nioge (ghuslu) ya Janaabah? Akasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ((Hapana, inatosha kwako kujimwagia viganja vitatu vya maji kichwani mwako na kisha jimwagie maji mwili mzima na baada ya kufanya hivyo utakuwa umeshasafishika)) [Ahmad na Muslim na Tirmidhiy akasema ni Hadiyth Hasan Sahihi]
سألت أسماء رضي الله عنها عن غسل الجنابة فقال: فقال (( تأخذ ماء فتطهر ، فتحسن الطهور ، أو تبلغ الطهور . ثم تصب على رأسها فتدلكه . حتى تبلغ شؤون رأسها . ثم تفيض عليها الماء)) . فقالت عائشة : نعم النساء نساء الأنصار ، لم يكن يمنعهن الحياء أن يتفقهن في الدين رواه الجماعة إلا الترمذي .
Asmaa رضي الله عنها alimuuliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم vipi kuoga Janaabah. Akasema: ((Achukue maji na kujisafisha, kwa kufanya wudhuu, kisha ajimwagie maji kichwani na asugue mpaka ahakikishe kuwa yamefika katika mizizi ya nywele na kisha ajimwagie maji mwili mzima)) Akasema 'Aishah: Uzuri wa wanawake ni wanawake wa Ki-Ansaar haiwazuii hayaa kujifunza dini yao [Imesimuliwa na kundi isipokuwa At-Tirmidhy]
Kwa hiyo ni dhahiri kutokana na Hadithi hizo kwamba mwanamke inapasa ahakikishe katika kuoga kwake maji yawe yanagusa ngozi ya kichwa chake, ikiwa ni kwa kujimwagia maji kichwani au kwa viganja vitatu vya maji vilivyojaa.
Ama kupangusa tu kichwa (Wiping) bila ya maji kufikia ngozi haifai kwani hii si maana ya 'Ghuslu'.
Kitaalamu: Tunapata hekma kwa maelezo yafuatayo.

Kama tulivyoona tafsiri ya Janaba ni hali anayokuwa nayo mtu baada ya kuingiliana mwanamke na mwanaume ama kuingiliana na kiumbe au kitu kingine au kutokwa na manii kwa hali yeyote.
Ifahamike kuwa manii si najisi kama ilivyo kwa Madhii, Madii na Mkojo. Kisheria nguo iingiapo manii yafaa kuswalia baada ya kuyakwangua au kuyafikicha kwa kukauka kwake ila si kwa Madii au Madhii na Mkojo.

ALLAH AALAM.
YAMEKUSANYWA NA SULEIMAN ABDALLAH.

Monday, April 11, 2011

Shetani huwa taabani mja anapoabudu,
tena hua mashakani tunapodumisha undugu,
mapenzi yetu waislamu humuongezea tabu,
hali yake huwa duni pale tunaposujudu,
kule kumtaja manani pekee tunamuadhibu,
tuzidishe ibada azidi kupata tabu,
itakapofika Qiyama peke yake apate tabu...
Amin Inshaallah
HAWA NDO BINADAMU: wakikukwepa usijali, ipo siku watakutafuta..
wakikusengenya nyamaza, huenda wakajifunza....
wakikununia omba Mungu, ipo siku watakuchekea....
wakikupongeza usiwaamini labda wanakutania....
wakikutenga achana nao, wao si kila kitu...
wakikudhulumu shukuru, Mungu atakulipa....
KUWA MAKINI KATIKA MAISHA YAKO!!
Think, how many stopped breathing since the year started?
how many bad accidents which left them disabled?
how many are lying in the hospitals with no hope of recovering?
how many are mad,eating from the garbage and sleepless?
WHY IT IS NOT YOU???
its time to say THANKS TO ALLAH cause he loves you and has made you strong while you did not even ask for it....
SAY ALHAMDULILLAH FOR EACH AND EVERYTHING ALLAH (S.W) GAVE YOU