MAKALA HAYA YANAENDELEA KUTOKA MAKALA YA KWANINI TUNAOGA JANABA
Manii si uchafu wa najisi kwa mjengo wake aliotuumbia Allah bali uchafu wa hali na kinai kwa ilipodondokea na hii ni kwa matashi ya binaadamu.
Turudi kutazama manii ni nini?
Manii ni kimiminika kijulikanacho na kubeba tafsiri ya lugha ya kitaalamu kama “SEMEN” kitolewacho (ifahamike manii hutolewa hayatoki yenyewe kama madii) na sehemu ya uume kwa mwanaume kama matokeo ya mshindo, mshushio, na upeo war aha na nakshi ya jimai ifahamikayo kitaalamu kama “Orgasm” na huwa na viambato na tabia zifuatazo:
A. Manii ndani yake kuna mbegu (sperms):
i. Mbegu hizi ndio asili ya uzazi na mjengo wa mwanaadamu zinatengenezwa katika makende (nje ya joto la ndani ya mwili). Mbegu hizi hujengwa na vitu viwili Chromosomes na gamates or male germ cells zenye Cytoplasm, vitu hivi viwili ni viambato vinavyopatikana katika vipimo vya DNA. (kuna X-chromosomes na Y-chromosemes)
ii. Katika mbegu hamna asili yeyote ya uchafu wala najisi bali katika vitu viwili tulivyovitaja hapo juu kuna vaiambato kama Vitamin (C&B12), Madini (Calcium, Magnesium, Pottasium, Phosphorus na Zinc) na Sukari(Fructose na Sorbito).
iii. Mbegu zenye manii ndizo zitolewazo, hazitoki zenyewe katika mwili wa mwanaume, sababu na kazi ya mbegu katika manii ni kupevusha mbegu za kike (Ova) katika jimai mgegu katika manii ni 10% tu.
iv. Mbegu (sperms) ifahamike kuwa ndani ya makende/korodani huhifadhiwa katika kiungo mfano wa koili kwa siku mwanaume mwenye afya hutengenza kati ya mbegu 70-150 milioni na huchukua wiki 10 mbegu 1 kupevuka na mbegu zilizopevuka katika koili hiyo hukaa takribani masiku 40 kabla ya kutolewa au kuvunjwavunjwa na kufyonzwa na mwili. Hapa tunajifunza na kugundua hamna haja ya kuzitoa mbegu kwa nji mbadala kama wanaotetea na kutoa elimu ya Punyeto, kwani Mola katuumba vema hamna haja ya kuvuka mipaka.Manii haijengwi na mbegu pekee bali pia kuna viambato kama ifuatavyo;
B. Manii pia ndani yake kuna kiambato krozomu kiitwacho “Seminal Plasma” kiambato hiki hutokana na maji yajijengayo na kutokana na damu ni kiambato kikubwa na muhimu katika manii huchukua zaidi ya 60% , kiambato hiki kipo katika hali ya kimiminika na hutolewa na tezi za mwanaume ziitwazo “Prostate Gland” zenye muundo wa “O” zizungukazo katika tundu mkabala na la mkojo. Kiamabato hiki hulinda mbegu na kuilisha kipindi cha safari yake ndefu mpaka katika mbegu za kike
NB: Eneo la mfumo wa uzazi wa mwanamke lina tindikali (acids) mno kwa kiwango ambacho seli za mbegu za kiume kuhimili maisha/kukaa na hivyo ndani ya “seminal Plazma” kuna viamabato vingi vya Alkalini vinavyoshindana na Acid ila ni kwa uchache mafanikio huwa na kwa namna hiyo mbegu chache hufika katika kupevusha yai la mwanamke, mara nyingi moja na kwa uchache mbili,tatu au nne kwa mapenzi ya Allah(sw).
Alkali iliyopo hapa hulinda gamets za kiume.
C. Manii pia ndani yake kuna tezi viambato ziitwazo “Seminal Vesicle” ambazo huyapa manii nguvu ya msukumo huyabeba seminal plasma tezi hizi hukaa pamoja na golegole /utelezi au kamasi/ute/utando utokanao na maji ya damu ambayo huizunguka mbegu ute huu ndio wenye protini kama chakula cha mbegu katika safari yake hadi katika ukuta wa uzazi.
Katika manii kuna viamabato kama “CITRIC ACID, “Kwa yakini mchanganuo wa kikemia wa kimiminika hiki manii, umedhihirisha kwamba pamoja na vitu vingine unahodhi kiwango kikubwa cha “phosphoric acid” na “calcic acid”. Na zote mbili hizi ni maada kima zenye taathira adhimu katika ujenzi wetu wa kimwili (kama wanadamu). Sodium na Zinc” pia kuna “Enzymes” hufanya sehemu ya asilimia zilizobaki, viamabato hivi utokaji wake hupita katika mishipa ya mwili na kuipasha ua kuichoma kwani vina moto na tindikali.
Nukta hii hutuleta Katika pointi ya msingi ya kujibu swali letu la msingi
Kwanini tunaoga Janaba?
“Kwanini tunaoga kwa kutokwa na manii ambayo si najisi”
Katika VIAMBATO hivi vya mwisho vya manii ndivyo hekma ya kitaalamu ya kupatikanika kuoga, kwani kwa athari ya mishipa ya mwili kuchomwa na maji ndicho kiungo pekee kinacho kuwa na uwezo wa kuipooza na kuipa nguvu yake ya asili, ifahamike kuwa :-
Kitaalamu maji ni muunganiko wa hewa mbili yaani “Hydrogen mbili (H2) na Oxygen moja (O) = H2O. Hivyo kwa zoezi la kushusha manii hufanya nguvu kutumika na husimamisha vinyweleo baada ya kumalizika zoezi lile katika kipindi hicho vinyweleo huwa wazi, hivyo unapooga maji hewa ile ya Oxygen na Hydrogen husafiri kwa kupitia vinyweleo kwenda kuiipooza mishipa na athari ya Acid na viambato vya mpito wa enzymes. Hivyo Allah akatutaka kuoga sio kuwa antuonea bali kwa kuwa ndiye aliye tuumba antufahamu na hatuna budi kuifuata amri yake hii ya sura ya 5 (Almaidah):6.
Acid hii ipatikanayo katika manii ni aina ya Citric yenye sifa za kelegeza baada ya kuchoma tokea yanapojikusanya hadi kutoka kwa aitoaye na inayemwingia pia hivyo hekma ya maji pia ni katika kurudisha nguvu ya mwili yaigusapo ngozi, Wataalamu wanatushauri kwa janaba tuoge maji ya kati yasiyo baridi sana kuliko ya moto kwalengo la kuirudisha hali ya mwili vema.
Hekma ya kutowaingilia wanawake nyuma na athari kwa Mashoga.
Wanaume wanaoingiliwa (mashoga) huathiriwa na kulegezwa na acid hii na pia kwa kupatikana virus wanaokosa mahali pakwenda kukaa hivyo hukosa haiba ya ukakamavu wa kiume na kuwa na haiba na mihemuko ya kike haya huwa matokeo ya athari za viambato alivyoumba mungu kwenda kukaa mahali Fulani kwenda kuwekwa kwengineko vivyo hivyo kwa wanawake waingiliwao nyuma Allah amekataza, kwa kufanya hivyo kitaalam kuna athari kubwa kwani hmna makazi sahihi ya viumbe/viambato alivyowaumba katika manii.
Kwanini manii si najisi?
Pia turejee swali letu linguine la msingi juu ya Utambuzi wa kunajisika manii:
“Je manii kwanini si najisi?”
Katika muda wa kipindi cha msisimko na hisia za kijinsia(mapenzi) na mahitajio pia wakati wa kufika kileleni manii husafirishwa na nguvu ya seminal vesicle tulizozizungumzia juu kama tezi viambato husafirishwa kwa njia ya mirija iitwayo “Vas Deferens” hivyo hayanajisiki kwa namna yeyote japo huonekana kutoka katika njia moja na mkojo, kinachofanyika kwa yale maji yanayotoka kabla ya manii yenyewe huwa najisi nay ale maji yanayotoka pekee bila manii huwa najisi vilevile(hapa ni katika pointi ya madhii na madii) kwa kupita njia isiyo mrija wa Vas Deferens. Katika njia ya Vas Deferens manii hupata kimiminika chenye kuwa na Sukari ya Fructose inayoongeza nguvu ya msukumo kama mafuta ya roketi (Bit like Roket fuel) na pia kuingiwa na tezi kama Prostate gland, Cowper gland pamoja na hiyo Seminal vesicle gland, tezi hizi hupunguza nguvu ya tindikali itokayo katika njia ya uchafu na nguvu ya mwili na pia mkojo hivyo kuifanya manii kuwa safi na salama itokapo, haiwezi kuwa najisi huu ndo ukweli juu ya manii kwa mujibu wa wataalamu pitia kitabu cha “Science; Spermatogenesis in Man, An Estimate of Its Duration” By Dr. C.G. Heller 1963 (Armenia medical Network) ..
ALLAH AALAM.
YAMEKUSANYWA NA SULEIMAN ABDALLAH.
TUWEKE MAZINGATIO
13 years ago
1 comment:
shukran sana kwa kutufaidisha na blog hii na inshaallah Allah awe ni mwenye kuwazidishia.
Post a Comment