SOMA UJIHESABU NAFSI YAKO.
1.Jee, umemdhukuru Mola na umemshukuru wakati wa kuamka kutoka usingizini?
2.Jee, umesali leo Sala ya Alfajiri Msikitini?
3.Jee, umesoma leo nyiradi za Asubuhi?
4.Jee, umemuomba siku ya leo Mola wako akuruzuku riziki ya halali?
5.Jee, umemshukuru Mola juu ya neema ya kuwa wewe ni Mwislamu?
6.Jee, umemshukuru Mola juu ya neema ya kuwa amekupa masikio na macho na moyo?
7.Jee, umekifungua leo kitabu cha Mola (Qur-ani) ukasoma baadhi ya Aya zake?
8.Jee, umemnasihi/umenasihi kuhusu mambo ya dini?
9.Jee, umemuomba Mola akuingize Peponi?
10.Jee, umejikinga kwa Mwenyezi Mungu akuepushe na Moto?
11.Jee, leo umesali Sala zako zote Msikitini?
12.Jee, leo umemsalia Mtume S.A.W.?
13.Jee, leo umeamrisha mema na kukataza mabaya?
14.Jee, leo ulikuwa na khushuu katika Sala zako unajua unayoyasema?
15.Jee, umependa kwa ajili ya Mola na kuchukia kwa ajili ya Mola?
16.Jee, leo umemuomba Mola msamaha akusamehe madhambi yako?
17.Jee, umemuomba Mola athibiti moyo wako juu ya dini Yake?
18.Jee, leo umemtabasamia katika uso wa ndugu yako Mwislamu.
19.Jee, umeusafisha ulimi wako kutokana na uongo, na kusema watu na kusema maneno ya upuuzi?
20.Jee, umeusafisha moyo wako kutokana na maradhi ya hasad n.k.
21.Jee, umeuzoesha moyo wako tabia njema kutokana na subira, uchaMungu, huruma kumtegemea Mola na ikhlaasi?
22.Jee, umekumbuka mauti na kaburi na siku ya Kiyama?
“FAHASABUU KABLA ANTUHASIBUU”
TUWEKE MAZINGATIO
13 years ago