بسم الله الرحمن الرحيم

kutafuta elimu ni faradhi kwa kila muislamu
الحمد لله الذي نستعينه ونستغفره ونعوذ بالله من شرور أنفسنا ومن سيئات أعمالنا من يهد الله فلا مضل له ومن يضلل فلا هادي له .



ونشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له ونشهد أن محمدا عبده ورسوله أرسله بالهدى ودين الحق ليظهره على الدين كله وكفى بالله شهيدا




Wednesday, April 13, 2011

KWANINI UISLAMU UMERUHUSU KUOA MKE ZAIDI YA MMOJA?.

Swali hili twaweza liuliza hivi: Kwanini wanawake hawafai kuolewa na mume zaidi ya mmoja,ila wanaume wamepewa ruksa ya wake wanne?
Hili linabainishwa kwa aya ya mwenyezimung ifuatayo:

[Anisaa:3]
“Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana”.
ALLAH ameruhusu mwanaume kuoa mke zaidi ya Mmoja na si mwanamke kuolewa na mwanamme zaidi ya mmoja kwani yeye(mwanamke )anahifadhi bacteria na virusi vinavyojengeka na mwili wa mwanadamu wapatikanao katika manii ya mwanaume na hivyo kimaumbile akihifadhi bacteria na virusi vya zaidi ya mwanamme mmoja ataleta madahara yafuatayo:
1. Ataleta mapiganao aya viumbe bacteria katika mfumo wake wa uzazi ulio na tabia ya kimaumbile kuyapokea na kuayahifadhi kupitia mfumo wake wa uzazi bacteria hawa ni pamoja na mjengo acidi uoneshao asili ya mwanadamu na kitambulisho cha mtu uitwao DNA(Deoxyribonucleic Acid) utaokanao na kujengwa na damu,mate na mbegu za kiume za mwanadamu. Bacteria hawa wakipigana hufa miongoni mwao kuleta uozo ujengao Neisseria gonorrhoeae na wengine hujengwa waitwao Chlamydia trachomatis, Treponema pallidum ,hukimbilia katika sehemu ya ndani ya mfumo wa uzazi kupitia nyama laini inayoujenga mfumo huo hivyo kuleta MAGONJWA kama klamadia,kaswende,kisonono na maumivu, hali hii na athari zake hujijenga na kuwa mabaya zaidi endapo itakuwa mapigano ya bacteria wa namna tofautitofauti kutokana na mwanamke kushiriki jimai na wanaume wengi.

2. Pia kutapatika muingiliano baina ya virusi mwili na kuzaliwa/ kujengwa virusi wapya wenye madhara waitwao kitaalamu herpes simplex virus(HSV) wasababishao ugonjwa wa malengelenge na hatari zaidi ni kupatiakana kwa Human immunodeficiency virus (HIV) washambuliao kingamwili.

Kulazimika kwa ndoa katika uislamu kuna hekma kubwa ambayo huyaepusha haya na pia kuyaepusha haya Allah (sw) amewalazimisha wanawake na wanaume kudumu katika jimai ya ndani ya ndoa. Mwanamke anapokea viambato vya mwanaume mmoja tu kwa namna ya maumbile aliyowaumbia Allah (sw) na sikinyume na hapo, kuyaasi haya ndipo zinakuja adhabu za mungu zinazotibika na zisizo na tiba kama UKIMWI.
Wataalamu wanasemaje katika uwezo wa uzalishaji na haja ya jimai:
Mwanaume wakawaida mwenye nguvu, mzima wa mfumo wa uzazi ana uwezo wa kuwahudumia wanawake watatu hadi wane kwa haja zote mbili za kuwatosheleza kwa mahitajio na akshi za kimwili pia kwa majenzi ya uzazi na kuzaliana, kwani wanaume wameumbiwa uwezo wa kutengeneza mbegu na mshindo wa jimai zaidi kuliko wanawake.
ALLAH AALAM.
YAMEKUSANYWA NA SULEIMAN ABDALLAH.

No comments: