HISTORIA FUPI YA IKHWAN MUSLIMIN/MUSLIM BROTHERHOOD-MISRI 1978-1938
Chama cha wanandugu wa kiislamu (Muslim brotherhood) kilianzishwa mwaka 1928 na Hassan Al-Banna ambaye kitaaluma ni mwalimu mwenye shahada.
Lengo kubwa la chama ni kuhamasisha /kushawishi watu waufuate utamaduni wa sheria za kiislam katika maisha yao ya kila siku pamoja na kutambua dhimma na wajibu wao katika kusimamia maamrisho ya Allah na kuwa mbali na makatazo yake. Haya yalikuja kutokana na uharibifu wa tamaduni za kiislam katika Misri na watu kupupia katika tamaduni za kimagharibi ambazo zililetwa na watawala wa kikoloni wa Misri. Mtazamo huu wa chama ulionekana kuwa ni kikwazo kwa utawala wa Misri kwa hiyo kilipata upinzani mkubwa sana kutoka kwa watawala ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kutishiwa kwa viongozi na wanachama wake na kutaifisha mali zao ili wasiendelee na kazi yao ya kuhamasisha na kuwaelimisha watu kurejea katika tamaduni za kiislam.
1939-1954.
Pamoja na upinzani alioupata kutoka kwa watawala,chama kiliendelea kukuwa kwa kasi na kufikia miaka ya 40, kilikadiriwa kuwa na wanachama zaidi ya milioni.
November mwaka 1948 kakika hali ya kushtukiza gari moja la Ikhwan lilivamiwa na polisi na katika upekuzi walioufanya walikuta nyaraka muhimu sana za chama miongoni mwazo ni zile zenyempango wa siri wa kijeshi wa chama ‘Secret Apparatus ;. Kufuatia kadhia hiyo viongozi 32 wa chama walikamatwa na kuzuiwa magerezani na ofisi kuwa katika ulinzi wa polisi huku hakuna ambacho kilikuwa kikiendelea. Mwezi uliofuata waziri mku wa Misri, Mamoud Fahmi Nolerash aliagiza kufutwa kwa chama cha Ikhwan katika Misri .
Kitendo ch waziri mkuu kutoa amri hiyo kiliwachukiza mno watu ,wanacham na wapenzi wake,Tarehe 28/12/1948 waziri mkuu aliulizwa na Abdul Mughrib Ahamad Hassan ,ni mwanachama wwa Ikhwan alionyesh kuchukizwa kwako na Jitihada za utawalw wa Misri dhidi ya Ikhwan.
Mwezi mmoja na nusu baadaye kiongozi wa ikhwan ImanHassan Al-Banna naye aliuliwa kwa kupigwa risasi katika viunga vya cairo na watu wanaodhaiwa ni mamluki wa serikali ya Misri;Na nafasi yake ikachukuliwa naJaji wa zamani,Hassn Ismail’l al-Hudeyb.
Meaka 1952 majengo zaidi ya 740 ya madanguro ,kumbi ,za starehe,makasino na mahoteli ambayo yalitumiwa sana na wazungu kama sehemu zao za kustarhe ,yaliharibiwa vibaya mno na kuteketezwa kabisa waliohusishw a na tukio hilo ni wan a ikhwan,Hakuna uthibitisho wa moja kwa moja juu ya tuhuma hizo kwa sababu yawezekana ni njama za serikali katika kukipaka matope chama hicho na wanachama wa ikhwan ili wapate sababu za kukihujumu,
1954-Present
Mwaka 1954 rais wa misri Gamal Abdul-Neer alinusurika kuuliwa katika jaribio lililofeli, na watuhumiwa njama hizo ni wale wana Ikhwan katika kitengo cha ‘Secret Apparatus’.
Kufuatia tukio hilo maelfu ya wanachama walikamatwa na kuzuiwa magerezani na katika kambi za mateso huku wakiteswa sana bila ya kufunguliwa mashtaka waliteswa kwa muda mrefu lakini mwaka 1964 baadhi ya wanachama waliuliwa akiwemo mwandishii maarufu wa kiislam Sayyid Qutub.lakin sayyid Qutub pamoja na kaka yake Muhammed Qutub walikamatwa tena maka 1965 mwezi wa Agosti,
Sayyid Qutub alikuwa mwanachama na kiongozi wa kiroho wa Ikhwan mwenye fikra pevu mno katika harakati za kuhuhisha uislam katika Misri.Fikra zake za kurejesha hadhi ya uislam na kuamsha hamasa kwa watu katika kukabili uislam kimatendo zilienea sana katika Misri .Lakini pamoja na hayo ndoto zake zilizimwa mwaka 1966 na serikali ya Misri pale alipohukumiwa kuuwawa.
Kifo cha Qutub kiliacha pengo kubwa mno kwa wana Ikhwan na waislam kwa ujumla kutokana na upevu wa fikra na mitizamo yake ya kiharakati,
Mwaka 1970,Rais wa Misri Anwar Sadat ambaye alimuita Gamal-Naseer, atoe amri ya kuachiwa kwa wanachama wa Ikhwan walioshikiliwa magerezani na aliwaomba wamsaidie katika kupambana na wapinzani wake wa kisiasa.Pamoja na mahusiao hayo mapya,chama cha Ikhwan kiliendelea na shughuli zake kwa kuvumiliwa mno na serikali ya Misri.Pamoja na uvumilivu huu hakikupata usajili ili kitambulikane kissheria.
Mwaka 1979 tarehe 6 ya mwezi October , Rais Anwaar Sadat, alikuwa adui mkubwa w aIkhwa na vyama vingine vya kiislam baada ya kusaini makubaliano y a amani na utawala wa Israel .Miaka miwili baadaye alkuja kuuwawa , tarehe 6 October 1981,na utawala kuchukuliwa na Hosni Mubarak.
Miaka ya 1980 katika utawala wa Mubarak wanafunzi na wataalam wengi wa kiislam walijiunga na Harkati za Ikhwan kwa pamoja waliweza kuunda vikundi mbalimbali vya wataalam na wanafunzi na kutengeneza mtandao madhubuti ambao ulijikita katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii kama elimu ,afya,mazingira, masuala y akiuchumi n.k.
Katika kipindi hiki pia chama cha Ikhwan kilipata nguvu kubwa mno ya kisiasa na kuonekana tishio kwa utawala uliopo madarakani.
Katika uchaguzi wa bunge mwaka 2005, wanchama wa Ikhwan waligombea kama wagombea binafsi kwa vile bado chama hakijasajiliwa serikalini ,walifanikiwaa kupata viti 88 ambavyo ni asilimia 20% ya viti vyote,wakati vyama vingine vyenye usajili viliambulia viti 14 tu.Haya yalikuwa ni mafanikio makubwa kwa Ikhwan japo kinaonekana na mizengwe mbalimbali ikiwemo kukamatwa kwa viongozi na wanachama wake ili kuwakatisha tama
Viongozi imara, mipango bunifu umadhubuti wa wanachama unafanya chama kuwa imara na kutekeleza majukumu yake.
Viongozi waliopata kuiongoza Ikhwan
1. Hassan Al-Banna –Mwanzilishi
2. Hassan Hudayb
3. Umar Al-Tilmisan
4. Muhammad Hamid Abu al-Nasr
5. Mustafa Mushhur
6. Ma’munAl-Hudayb
7. Mahmoud alMahdy Akif
8. Muhamad Badie----hadi sasa.
TUWEKE MAZINGATIO
13 years ago
No comments:
Post a Comment